Ulazima wa funga unaanza pale kunapopambazuka alfajiri ya pili. Nao ni ule weupe unaoonekana katika upeo wa macho na inamalizika kwa kuzama kwa jua. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ

“Sasa waingilieni… “

Bi maana wake.

وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ

“… na tafuteni yale Allaah amekuandikieni.”

Maana ya maneno:

يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“… ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi… “[1]

kubainike weupe wa mchana kutoka katika giza la usiku.

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/374)
  • Imechapishwa: 22/03/2021