Anaomba kuwa mkuu wa kituo cha dini

Swali: Mtu akiomba awe mkuu wa masomo au mwenye kuyawakilisha. Je, maombi yake haya yanazingatiwa ni kuomba uongozi?

Jibu: Ndio. Hakuna neno akiwa anahisi ndani ya nafsi yake kutosheleza na akatambua kuwa ni mwenye manufaa na kunufaisha zaidi kuliko wengine. Ni kama ambavo Yuusuf alivoomba uongozi na akasema:

اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ

“Niweke katika kusimamia hazina ya nchi, kwani hakika mimi ni mchungaji mjuzi.”[1]

Lakini akiwa hahisi ndani ya nafsi yake kutosheleza basi ni mwenye kuidhulumu nafsi yake. Haifai kwake kuomba kitu hicho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Abu Dharr:

“Mimi nakupenda na nakuona kuwa ni mnyonge. Hivyo basi, usiongoze kati ya watu watu wawili na wala usisimamie mali ya yatima.”

Yeye anaitambua zaidi nafsi yake. Akiwa anaona kuwa anafaa na anaweza kutoa manufaa na pia atawalazimisha walioko chini yao kushikamana na maamrisho ya Allaah, basi ni kitu kizuri. Lakini akiwa ni mnyonge, hawezi kusimamisha amri za Allaah na wala kutekeleza mambo ya wajibu, basi huyo atakuwa ni mwenye kuidhulumu nafsi yake.

[1] 12:55

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 22/03/2021