Kufunga Ramadhaan ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu na faradhi kutoka kwa Allaah inayotambulika vyema katika dini. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu.”[1]

mpaka aliposema:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo la batili. Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[2]

Mmeandikiwa (كتب) maana yake ni kwamba mmefaradhishiwa. Maneno Yake:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[3]

ni amri ya ulazima.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu umejengeka juu ya vitano… “

Akataja miongoni mwavyo:

“Kufunga Ramadhaan.”[4]

Hadiyth kuhusu dalili juu ya ulazima wake ni nyingi na zenye kutambulika.

Waislamu wamefikiana juu ya ulazima wake. Ambaye ataikanusha basi amekufuru.

[1] 02:183

[2] 02:185

[3] 02:185

[4] al-Bukhaariy (08) na Muslim (111).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/373)
  • Imechapishwa: 22/03/2021