Allaah (Subhaanah) ameeleza kuhusu watu ambao wako na elimu lakini hata hivyo haikuwafaa kitu elimu yao. Hii ni elimu yenye manufaa yenyewe kama yenyewe, lakini haikumnufaisha kitu mwenye nayo. Amesema (Ta´ala):

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا

“Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwavikubwa.”[1]

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ

“Wasomee habari za yule Tuliyempa Aayah Zetu akajivua nazo. Shaytwaan akamfuata na [hatimaye] akawa miongoni mwa waliopotoka. Lau Tungelitaka tungelimnyanyua [kutoka utwevuni] kwazo [hizo Aayah], lakini aligandamana na dunia na akafuata matamanio yake.”[2]

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ

”Basi wakafuatia baada yao kizazi kibaya waliorithi Kitabu; wanachukua anasa za hapa duniani na wanasema: “Tutasamehewa na inapowafikia tena anasa kama hizo wanazichukua.”[3]

أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

“Je, umemuona yule aliyejifanyia matamanio yake kuwa ndio mungu wake na Allaah akampotoa juu ya kuwa na elimu na akapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake na akaweka kizibo juu ya macho yake? Basi nani atamwongoza baada ya Allaah? Ni kwa nini hamkumbuki?”[4]

[1] 62:05

[2] 07:175-176

[3] 7:169

[4] 45:23

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 34
  • Imechapishwa: 09/09/2021