Himdi zote njema anastahiki Mola. Swalah na amani nyingi zimwendee Muhammad , kizazi chake na Maswahabah zake wote.

Hiki hapa ni kijitabu kifupi juu ya maana ya elimu, mafungu yake katika elimu yenye manufaa na elimu isiyokuwa yenye manufaa pamoja na uzindushi juu ya kwamba elimu ya Salaf ndio bora kuliko elimu ya wale waliokuja nyuma. Namwomba Allaah msaada, nakiri ya kwamba hapana nguvu wala namna pasi Naye na nasema:

Wakati fulani Allaah (Ta´ala) huitaja elimu kwa njia ya kuisifia. Katika hali hii inakuwa ni elimu yenye manufaa. Wakati mwingine Huitaja kwa njia ya kuisimanga. Katika hali hii inakuwa ni elimu isiyokuwa na manufaa.

Amesema (Ta´ala) kuhusu sampuli ya elimu ya kwanza:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ

“Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu.”[1]

شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلا هُوَ وَالْمَلائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِماً بِالْقِسْطِ لا إِلَهَ إِلا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

“Allaah ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye na Malaika, na wenye elimu [wote wameshuhudia kwamba Yeye] ni Mwenye kusimamisha [uumbaji Wake] kwa uadilifu – hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye; Mwenye nguvu zisizoshindikana, Mwenye hekima.”[2]

وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا

“Sema: ”Mola wangu! Nizidishie elimu.”[3]

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si venginevo wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”[4]

Vilevile Allaah (Subhaanah) amesimulia namna alivyomfunza Aadam majina ya vitu kisha baadaye akawaamrisha Malaika wataje majina yavyo ambapo wakajibu:

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

“Wakasema: “Utakasifu ni Wako hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza, hakika Wewe ni Mjuzi wa yote, Mwenye hekima wa yote.”[5]

Pia Allaah (Subhaanah) ametaja jinsi Muusa alivyomwambia al-Khadhwir (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam):

هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا

“Je, nikufuate ili unifunze katika yale uliyofunzwa ya busara?”[6]

Yote haya inahusiana na elimu yenye manufaa.

[1] 39:09

[2] 03:18

[3] 20:114

[4] 35:28

[5] 2:32

[6] 18:66

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 09/09/2021