01. Wenye kushika sana duniani ndio wenye njaa sana Aakhirah

1 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ahmad bin Muhammad bin ´Umar bin Abaan al-´Abdiy ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Ubayd al-Qurashiy ametuhadithia: Mansuur bin Abiy Muzaahim ametuhadithia: Yahyaa bin Hamzah ametuhadithia, kutoka kwa Thawr bin Yaziyd, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan na Habiyb bin ´Ubayd ar-Rahbiy: al-Muqdaam bin Ma´d Yakrab ametuhadithia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanadamu hajapatapo kujaza chombo kibaya kama tumbo. Inatosha kwa mtu kuchukua matonge kadhaa kwa ajili tu ya kusimamisha mgongo wake. Ikiwa mwanadamu hana budi, basi theluthi iende katika chakula, theluthi iende kwenye kinywaji na theluthi iende kwenye pumzi.”[1]

2 – Abu ´Aliy al-Hasan bin ´Arafah ametuhadithia: Abu ´Aaswim al-´Abbaadaaniy ametuhadithia, kutoka kwa al-Muhabbar bin Haaruun, kutoka kwa Abu Yaziyd al-Madiyniy, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Muraqqa´, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hajaumba chombo ambacho kikijaa ni kibaya kama tumbo. Akiwa hana hana budi, basi afanye theluthi iwe ya chakula, theluthi iwe ya kinywaji na theluthi iwe ya pumzi.”

3 – al-Hasan bin as-Sabbaah ametuhadithia: Sa´iyd bin Muhammad ametuhadithia, kutoka kwa Muusa al-Juhaniy, kutoka kwa Zayd bin Wahb, ambaye amesema:

”Salmaan alilazimishwa kula chakula ambapo akasema: ”Inatosha, inatosha. Nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Hakika watu wanaoshiba sana duniani ndio wataokuwa na njaa sana Aakhirah. Ee Salmaan! Hakika dunia ni gereza ya muumini na Pepo ya kafiri.”[2]

4 – al-Hasan bin [tupu] amenihadithia [tupu] ´Abdullaah [tupu], kutoka kwa Abur-Rajaa’, kutoka kwa mtu aliyemsikia Abu Juhayfah, kutoka kwa Abu Juhayfah, ambaye ameeleza:

”Alitoa bweu katika kikao cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambapo akasema: ”Acha kutoa bweu. Hakika watu wataokuwa na njaa sana siku ya Qiyaamah ni wale waliokuwa wakishiba sana duniani.” Abu Juhayfah amesema: ”Sijala nikashiba tokea miaka thelathini.”[3]

[1] at-Tirmidhiy (2456) ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[2] Ibn Maajah (3351). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (2722) kwenda mpaka kwa “… ndio wataokuwa na njaa sana Aakhirah.” Kipande kingine kimepokelewa na Muslim (2956) na at-Tirmidhî (2324).

[3] Tazama ”as-Swahiyhah” (2/672-677)

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 23-27
  • Imechapishwa: 05/06/2023