01. Siri ya wanamme kufanywa wasimamizi na kuwa bora

Allaah (Ta´ala) amesema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”[1]

Ibn Kthiyr amesema:

“Bi maana mwanamme ni msimamizi wa mwanamke. Kwa maana nyingine yeye ndiye kiongozi wake, mkubwa wake, mwenye kumuhukumu na mwenye kumuadabisha anapokengeuka.”[2]

as-Sa´diy amesema:

وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“… na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”

Bi maana kwa sababu ya ubora wa wanamme kwa wanawake na kufadhilishwa kwao juu yao. Mwanamme kufanywa kuwa bora juu ya mwanamke ni kwa sampuli nyingi; uongozi umefanywa ni kitu maalum kwa wanamme, unabii na utume. Vilevile wamefanywa maalum kwa ´ibaadah nyingi; Jihaad, idi na swalah ya ijumaa. Yako mengine ambayo Allaah amewafanya kupwekeka nayo kama vile akili, subira na ustahamilivu ambao haupatikani kwa wanawake. Vivyo hivyo wamepwekeshwa kuwasimamia wanawake kwa matumizi. Bali kuna matumizi mengi ambayo wamepwekeka nayo wanamme na wanatofautiana kutokana na wanawake. Na pengine hiyo ikawa ndio siri ilioko nyuma ya maneno Yake:

وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“… na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”

inayofahamisha matumizi aina yote. Kwa hiyo hayo yote yakajulisha ya kwamba mwanamme ni kama mtawala na kiongozi kwa mke wake. Mwanamke ukimlinganisha na mume ni kama mtumwa wake. Kazi ya mume ni kusimamia kile ambacho Allaah amempa kukisimamia na kazi ya mke ni kusimamia kazi ya kumtii Mola Wake na kumtii mume wake.”[3]

al-Qaasimiy amesema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake.”

Wingi wa usimamizi. Ni yule ambaye anasimamia manufaa, uendeshaji na kuadabisha.  Kwa maana nyingine ni kwamba wamesalitishwa kuwaadabisha wanawake na kuwasimamia hali ya kuwaamrisha na kuwakataza. Ni kama mtawala anavowasimamia wananchi wake. Hilo ni kutokana na mambo mawili:

1 – Kuna ambalo wametunukiwa.

2 – Kuna ambalo wamechuma.

Ameashiria hilo la kwanza pale aliposema (Subhaanah):

بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ

“Kwa kuwa Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine.”

Dhamira inarudi kwa wanaume na wanawake wote wawili. Kwa msemo mwingine ni kwamba wanamme wamekuwa wenye kuwatawala wanawake kwa sababu ya Allaah kuwafadhilisha baadhi – nao ni wanamme – juu ya wengine – nao ni wanawake. Ameashiria hilo la pili pale aliposema (Subhaanah):

وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“… na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”

na katika mahari na matumizi wanayotoa.”[4]

[1] 04:34

[2] Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym (01/194).

[3] Taysiyr-ul-Kariym ar-Rahmaan (01/344).

[4] Mahaasin-ut-Ta´wiyl (05/130) kwa kifupi.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 04-07
  • Imechapishwa: 14/09/2022