00. Kitabu kifupi kimaneno, muhimu katika maudhui yake

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye, kumuomba msaada na msamaha. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu. Yule aliyeongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha, na yule aliyepotoshwa na Allaah, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yu peke yake pasi na mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Amma ba´d:

Hiki ni kijitabu ”Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah” ambacho ni kifupi katika maneno yake lakini muhimu katika maudhui yake na chenye faida kubwa. Nimepanga milango yake ifuatavyo:

1 – Ukubwa wa haki ya mume.

2 – Mahimizo ya kumtii mume.

3 – Khatari ya kumkasirisha mume, kwenda kinyume na amri yake na kupoteza haki zake.

4 – Fadhilah za mke mwema.

5 – Sifa za mke mwema.

6 – Mambo yanayomsaidia mke kupata sifa hizi.

Namuomba Allaah (´Azza wa Jall) awanufaishe nacho dada zetu waislamu, kila mwenye kukisoma na akifanye ni takasifu kwa ajili ya uso Wake. Kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kutoa, Mkarimu.

Imeandikwa na;

Muhammad Shuwmaan

01 Dhul-Qa´dah 1410

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 03-04
  • Imechapishwa: 14/09/2022