Ni ´Abdullaah bin az-Zubayr bin ´Iysaa bin ´Ubaydillaah bin Usaamah bin ´Abdillaah bin Humayd bin Zuhayr bin al-Haarith bin Asad bin ´Abd-il-´Uzza.

Kuna maoni yanayosema kuwa babu yake ni ´Iysaa bin ´Abdillaah bin az-Zubayr bin ´Ubaydillaah bin Humayd. al-Humaydiy ni Imaam, Haafidhw, Faqiyh na Shaykh wa Makkah; Abu Bakr al-Qurashiy, al-Asadiy, al-Humaydiy na al-Makkiy. Mtunzi wa “al-Musnad”.

Amehadithia kutoka kwa Ibraahiym bin Sa´d, Fudhwayl bin ´Iyaadhw na Sufyaan bin ´Uyaynah, ambaye alipokea sana kutoka kwake na akafanya vizuri, al-Waliyd bin Muslim, Marwaan bin Mu´aawiyah, Wakiy´ na ash-Shaafi´iy. Hakupokea sana lakini hata hivyo ana utukufu na heshima katika Uislamu.

Amehadithia kutoka kwake al-Bukhaariy, ad-Dhuhliy, Salamah bin Shu´ayb, Ya´quub al-Fasawiy, Abu Zur´ah ar-Raaziy, Bishr bin Muusa, Abu Haatim, Ya´quub bin Shaybah, Abu Bakr Muhammad bin Idriys al-Makkiy na alikuwa akiandika na wengineo.

Ahmad bin Hanbal amesema:

“Tunamzingatia al-Humaydiy kuwa imamu.”

Abu Haatim amesema:

“Mtu ambaye ni imara zaidi kwa Ibn ´Uyaynah ni al-Humaydiy. Yeye ndiye kiongozi wa wanafunzi wa Ibn ´Uyaynah. Ni imamu mwaminifu.”

Abu Ya´quub al-Fasawiy amesema:

“al-Humaydiy ametuhadithia na sijaona mtu ambaye anautakia Uislamu na waislamu kheri zaidi kuliko yeye.”

Muhammad bin Ishaaq al-Marwaziy amesema:

“Nimemsikia Ishaaq bin Raahuuyah akisema: “Maimamu katika zama zetu ni ash-Shaafi´iy, al-Humaydiy na Abu ´Ubayd.”

´Aliy bin Khalaf amesema:

“Nimemsikia al-Humaydiy akisema: “Hakuna yeyote atakayetushinda muda wa kuwa mimi niko Hijaaz, Ahmad bin Hanbal ´Iraaq na Ishaaq [bin Raahuuyah] Khuraasaan.”

Abul-´Abbaas as-Saraaj amesema:

“Nimemsikia Muhammad bin Ismaa´iyl akisema:

“al-Humaydiy ni imamu katika Hadiyth.”

Muhammad bin Sa´d amesema:

“´Abdullaah bin az-Zubayr al-Asadiy al-Humaydiy anatokana na kizazi cha Asad bin ´Abil-´Uzza bin Qusway, mwanafunzi wa Ibn ´Uyaynah na amepokea kwake, amekufa Makkah mwaka wa 219. Alikuwa mwaminifu na anayehifadhi sana.”

Vivyo hivyo ndivo alivosema al-Bukhaariy katika “Taariykh” kuhusu kufa kwake. Wengine wakasema kuwa amekufa mwaka wa 220.

Muslim amepokea kutoka kwake katika utangulizi wa kitabu chake, Ibn Maajah katika “at-Tafsiyr” na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (10/626-621)
  • Imechapishwa: 13/09/2022