Himidi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, ambaye ndiye Mtume wa mwisho, na kila yule ambaye atashikamana na Sunnah zake na akapita katika njia yake mpaka siku ya Qiyaamah.
Ama baada ya hayo;
Hakika ´Aqiydah ndio msingi ambao juu yake hujengwa maendeleo ya mataifa. Ufanisi na ustawi wa kila taifa unahusiana moja kwa moja na usahihi wa ´Aqiydah yake na fikira yake. Kwa sababu hii nyujumbe za Mitume wote (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam) zimekuja kulingania ´Aqiydah. Kila Mtume alikuwa akianza kuwalingania wafuasi wake kwa kuwaambia:
اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ
“Mwabuduni Allaah, kwani hamna mungu wa haki mwengine asiyekuwa Yeye.” (al-A´araaf 07:59)
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.”” (an-Nahl 16:36)
Hivyo ni kwa sababu Allaah (Subhaanah) amewaumba viumbe ili wamuabudu Yeye Mmoja asiyekuwa na mshirika. Amesema (Ta´ala):
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
”Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu.” (adh-Dhaariyaat 51:56)
´Ibaadah ni haki ya Allaah juu ya waja Wake. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh):
“Je, wewe unajua ni ipi haki ya Allaah juu ya waja wake na ni ipi haki ya waja juu ya Allaah? Akasema: “Haki ya Allaah juu ya waja Wake ni wamuabudu Yeye na wala wasimshirikishe Yeye na chochote. Na haki ya waja juu ya Allaah ni kutomuadhibu yule ambaye hakumshirikisha Yeye na chochote.”[1]
Hii ndio haki ya kwanza. Haitanguliwi na chochote na wala haitanguliwi na haki ya yeyote. Amesema (Ta´ala):
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
”Na Mola wako ameamrisha ya kwamba, msiabudu yeyote isipokuwa Yeye pekee. Na kuwatendea wema wazazi wawili.” (al-Israa 17:23)
قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
”Sema: “Njooni nikusomeeni yale aliyoyaharamisha Mola wenu kwenu kwamba: Msimshirikishe na chochote na muwafanyie wema wazazi wawili… ” (al-An´aam 06:151)
Kwa sababu haki hii ina umuhimu wa pekee na ni ya kwanza kabla ya haki nyingine zote, na kwa kuwa ni msingi ambao hukumu zote za dini hujengwa juu yake, tunamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikaa Makkah kwa miaka kumi na tatu akiwalingania watu kusimamisha ´ibaadah hii ya Tawhiyd na kuondoa ushirikina. Isitoshe sehemu kubwa ya Qur-aan Tukufu imejaa Ayah nyingi zinazothibitisha jambo hili na kuondoa shaka zote zinazohusiana nayo. Aidha kila anayeswali, iwe ni swalah ya faradhi au Sunnah, anampa Allaah ahadi ya kusimamisha ´ibaadah hii pale anaposema:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
”Wewe pekee tunakuabudu na Wewe pekee tunakuomba msaada.”
(al-Faatihah 01:05)
Haki hii kubwa inaitwa Tawhiyd-ul-´Ibaadah, Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah au upwekeshaji katika nia na makusudio. Majina yote haya yana maana moja. Jengine ni kwamba Tawhiyd hii iko katika maumbile ya mwanadamu:
“Kila mtoto huumbwa juu ya maumbile…”
Hakika hapana vyenginevyo kupondoka kutokana nayo kunatokana na malezi mabaya.
”… wazazi wake ndio humfanya ima akawa myahudi, mnaswara au mwabudia moto.”[2]
Tawhiyd hii ni jambo la asili kwa walimwengu na shirki imejitokeza na kujipenyesha ndani yake. Amesema (Ta´ala):
كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ
“Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah akawatuma Mitume hali ya kuwa ni wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu kati ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo.” (al-Baqarah 02:213)
وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا
“Na wala watu hawakuwa isipokuwa ni ummah mmoja, kisha wakakhitilafiana.” (Yuunus 10:19)
Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):
”Baina ya Aadam na Nuuh (´alayhimaas-Swalaatu was-Salaam) kulipita karne kumi. Wakati huo watu wote walikuwa katika Uislamu.”[3]
´Allaamah Ibn-ul-Qayyim amesema:
”Haya ndio maoni sahihi kuhusu Aayah iliyotangulia.”
Isitoshe akataja Aayah zinazoipa nguvu katika Qur-aan[4].
Haafidhw Ibn Kathiyr ameisahihisha katika Tafsiyr yake ya Qur-aan.
[1] al-Bukhaariy (300/13) katika “at-Tawhiyd” na Muslim katika “al-Iymaan” (30).
[2] Muslim (2047).
[3] Tafsiyr ya Ibn Kathiyr (1/250)).
[4] Ighaathat-ul-Lahfaan (02/201)).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 03-06
- Imechapishwa: 01/01/2025

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 03-06
Imechapishwa: 01/01/2025
https://firqatunnajia.com/01-haki-ambayo-haitanguliwi-mbele-ya-haki-ya-mwengine-yeyote/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)