Shirki ilianza kuzuka kwa watu wa Nuuh wakati walipochupa mipaka kwa watu wema na wakafanya kiburi kwa uligano wa Mtume wao:
وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا
”Wakasema: “Msiwaache waungu wenu – na wala msimwache Wadd na wala Suwaa´ na wala Yaghuuth na Ya’uuq na Nasr!” (Nuuh 71:23)
al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema katika ”as-Swahiyh” yake[1] kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):
”Haya ni majina ya watu wema kutoka kwa watu wa Nuuh. Wakati walipofariki shaytwaan akawaendea watu wake na kuwaambia watengeneze picha na waziweke katika majlisi zao walipokuwa wakikaa ili wawakumbuke na waziite kwa majina yao. Wakafanya hivyo. Hawakuziabudu papohapo; mpaka walipofariki watu wale na elimu ikasahaulika ndipo wakaabudiwa.”
Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
”Wamesema si zaidi ya mtu mmoja katika Salaf kwamba wakati walipofariki walikuwa wakikaa muda mrefu kwenye makaburi yao, kisha wakatengeneza picha zao. Kisha kukapita muda mrefu ndipo wakawaabudu.”[2]
Kisha akaendelea kusema (Rahimahu Allaah):
”Shaytwaan ameweza kucheza na washirikina katika kuabudu masanamu katika kila ummah kwa kadiri ya akili zao. Baadhi yao amewalingania katika kumuabudu kwa njia ya kumuadhimisha maiti ambaye wametengeneza picha yake kwa sura yake, kama ilivyokuwa kwa watu wa Nuuh. Sababu hii hutokea mara nyingi kwa washirikina wa kawaida. Ama washirikina wenye kujitambua wanadai eti kuchukua masanamu kwa sura ya sayari zinazoathiri katika ulimwengu, wakazitengenezea nyumba, bustani, pazia na vichinjwa. Haya bado ni yenye kuendelea ulimwenguni, ni mamoja hapo zamani mpaka hivi sasa.
Msingi wa madhehebu haya ni kutoka kwa washirikina wa wakisabai, ambao ni watu wa Ibraahiym (´alayhis-Salaam) ambao alijadiliana nao katika kusambaratisha shirki na kuvunja hoja zao kwa elimu na miungu yao kwa mkono wake. Wakaamua kumchoma moto.
Kundi jengine wakachukua mwezi na kuufanya kuwa sanamu. Wakadai kuwa unastahiki kuabudiwa na kwamba ndio unaopeleka huu ulimwengu ulio chini.
Kundi jengine likaabudu moto, nao ni wale waabudia moto. Wakaunjengea nyumba nyingi, wakauwekea watunzaji, walinzi na wasimamizi na kuhakikisha kuwa ´ibaadah yao haikatiki hata mara moja.
Kundi jengine likaabudu maji ambao wakadai kwamba maji ndio chanzo cha kila kitu, sababu ya kuzaliwa, ukuaji, ujenzi, usafi na ustawi wa maisha.
Kundi jengine likaabudu wanyama, kundi jengine likaabudu farasi, kundi jengine likaabudu ng´ombe, kundi jengine likaabudu mtu aliyehai na aliyekufa, kundi jengine likaabudu jini, kundi jengine likaabudu mti, kundi jengine likaabudu Malaika.”[3]
[1] al-Bukhaariy (06/133).
[2] Ighaathat-ul-Lahfaan (02/202).
[3] Ighaathat-ul-Lahfaan (2/218, 219, 230, 231, 233)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 06-08
- Imechapishwa: 01/01/2025

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 06-08
Imechapishwa: 01/01/2025
https://firqatunnajia.com/02-sababu-ya-kuzuka-shirki-ulimwenguni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)