01. Hadiyth “Ee Bilaal! Nieleze ni kitendo gani unachokitaraji zaidi katika Uislamu… “

226 – Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Bilaal:

يا بلالُ! حَدِّثْني بأرجى عملٍ عمِلته في الإسلام؛ فإنّي سمعتُ دَفَّ نعلَيك بين يَديَّ في الجنةِ” . قال: ما عملتُ عملاً أرجى عندي من أنّي لم أتطهَّر طُهوراً في ساعةٍ من ليلٍ أو نهارٍ إلا صلّيتُ بذلك الطُّهورِ ما كُتب لي أنْ أصلي

“Ee Bilaal! Nieleze ni kitendo gani unachokitaraji zaidi katika Uislamu. Kwani hakika mimi nimesikia nyayo za viatu vyako mbele yangu Peponi.” Akasema: “Sijafanya kitendo ninachokitaraji zaidi kuliko kuwa sijawahi kujitwahirisha, pasi na kujali ni saa ya usiku au mchana, isipokuwa huswali kwa twahara hiyo kile niliachoandikiwa kukiswali.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/210)
  • Imechapishwa: 25/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy