01. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini kuwa Allaah (Ta´ala) amepwekeka juu ya kuumba, uola na uendeshaji wa mambo. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anaufunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na [ameumba] jua na mwezi na nyota vyote vimetiishwa kwa amri Yake. Zindukeni! Ni Vyake pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.” (07:54)

لِّلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ

“Ni wa Allaah pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba atakavyo.” (42:49)

لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi, anahuisha na anafisha, Naye juu ya kila jambo ni muweza.” (57:02)

Tawhiyd hii inaitwa Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na imekita katika nafsi ya kila mwanadamu. Hakuna mwanadamu yeyote anayepingana nayo, ni mamoja awe muislamu au kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu makafiri:

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ

“Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” (31:25)

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ

“Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.” (12:106)

Mujaahid (Rahimahu Allaah) amesema:

“Wanaamini kuwa Allaah ndio muumbaji na mruzukaji wao anayewafisha. Hii ndio imani yao pamoja na kuwa wanamshirikisha na wengine.”

Washirikina walikuwa hawaitakidi kuwa waungu wao wana sehemu katika uumbaji wa Allaah. Walikuwa wakiamini kuwa Allaah ndiye mwenye kuendesha hayo peke yake. Pamoja na hivyo walikuwa wakisema wanafanya Tawassul kupitia wao ili kuweza kumfikia Allaah na wawashufaie  mbele Yake. Amesema (Ta´ala):

أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ ۚ وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Zindukeni! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika. Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi [husema]: “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.”” (39:03)

قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ ۚ بَلْ إِن يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا

“Sema: “Je, mnawaona washirika wenu ambao mnawaomba badala ya Allaah nionyesheni ni nini walichoumba katika ardhi au wana ushirika wowote mbinguni au Tumewapa kitabu chochote kile, kisha wao kwa hicho wakawa na hoja  za wazi?” Hapana! Bali hawaahidiani madhalimu wao kwa wao isipokuwa uongo mtupu.” (35:40)

إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ

“Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: “hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah” basi wanatakabari na wanasema: “Je, sisi kweli tuache miungu yetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?”” (37:35-36)

أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ

“Amewafanya miungu wote kuwa ni mungu mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno!” (38:05)

Allaah (Ta´ala) alithibitisha Tawhiyd hii ili ihakikishwe, ithibitike na kumwelekeza mtu katika uwajibu wa Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah, kwa sababu Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni yenye kulazimisha mtu asimwabudu yeyote isipokuwa Allaah (Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambae amekuumbeni na wale wa kabla yenu ili mpate kuwa na uchaji.” (02:21)

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ

“Huyo ndiye Mola wenu pekee, Anao ufalme, hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Yeye, basi vipi mnageuzwa?” (39:06)

فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ

“Basi wamwabudu Mola wa nyumba hii, Ambaye anawalisha kutokana na njaa na akawapa amani kutokana na khofu.” (106:03-04)

Allaah (Ta´ala) amesema kwamba Yeye peke yake ndiye Mwenye kuwaumba na Mwenye kuwaruzuku, jambo ambalo hawana shaka nalo. Amefanya hilo kuwa ni hoja dhidi yao ili iwe ni wajibu kumwabudu yeye peke yake, hali ya kuwa hana mshirika. Allaah (Ta´ala):

قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَىٰ ۗ آللَّـهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا شَجَرَهَا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًاۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚقَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Sema: “Sifa zote kamilifu na tukufu anastahiki Allaah na amani kwa waja Wake ambao amewachagua!” Je, Allaah ni bora au wale wanaowashirikisha? Au nani aliyeumba mbingu na ardhi na akakuteremshieni kutoka mbinguni maji, kisha tukaotesha kwayo mabustani anisi za kupendeza kabisa, nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko mungu mwengine wa haki pamoja na Allaah? – Bali wao ni watu wanaosawazisha. Au nani aliyeijaalia ardhi kuwa mahali pa matulio na akajaalia baina yake mito na akaiwekea milima na akajaalia baina ya bahari mbili kizuizi. Je, yuko mungu mwengine wa haki pamoja na Allaah? Bali wengi wao hawajui. Au nani anayemuitika aliyedhikika anapomwomba na akamuondoshea dhiki na akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mungu mwengine wa haki pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. Au nani anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari na nani anayetuma pepo za bishara kabla ya rehema Zake. Je, yuko mungu mwengine wa haki pamoja na Allaah? – Ametukuka Allaah kutokamana na yale wanayomshirikisha.” (27:59:63)

Katika Aayah zote hizi Allaah (Ta´ala) anawakemea washirikina wanaokiri kuwa Allaah (Ta´ala) peke yake ndiye muumbaji wa mbingu na ardhi na mwenye kunufaisha na kudhuru. Pamoja na hivyo kukiri kwao huku hakukuwanufaisha kitu, kwa sababu walimshirikisha Allaah pamoja na waungu wengine ambao walikuwa wakiwaabudu kama wanavyomuabudu Allaah. Hakika nadharia hii inaenda kinyume na Shari´ah na akili. Ambaye amepwekeka katika mambo yote haya – kama kuumba, kuruzuku, kuhuisha na kufisha – ndiye mwenye haki ya kutekelezewa utiifu aina yote. Ndio maana Allaah (Ta´ala) amewakemea pale aliposema:

أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ

“Je, yuko mungu mwengine wa haki pamoja na Allaah?”

Hata hivyo hakusema:

“Je, kuna muumbaji mwengine pamoja na Allaah,” kwa sababu walikuwa ni wenye kuthibitisha hili.

Allaah (Ta´ala) amebainisha ni ubatilifu uliyoje kuwa na mshirika katika uola. Lau angelikuwepo mwengine aliye na sehemu katika hilo, basi mbingu na ardhi vingeharibika. Hili ni lenye kufahamika pia kwa akili ya kimaumbile. Allaah (Ta´ala):

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ

“Allaah hakujifanyia mwana yeyote na wala hakukuwa pamoja Naye mungu yeyotehapo bila shaka kila mungu angelichukua vile alivyoviumba na bila shaka baadhi yao wangeliwashinda wengineo. – Utakasifu ni wa Allaah kutokana na yale wanayoyaelezea.” (23:91)

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا

“Lau wangelikuweko humo miungu mingi asiyekuwa Allaah, bila shaka zingelifisidika.” (21:22)

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 12-16
  • Imechapishwa: 20/06/2020