Tambua ya kwamba Allaah ametutunuku neema zisizohesabika. Yule ambaye anaweza kujua ni ngapi ni Allaah ambaye ametuongoza katika Uislamu na akatufanya kuwa katika Ummah bora kabisa. Mitume wote (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) walipata sifa maalum na Mtume wetu alipata kila kitu na zaidi. Yeye ndiye wa kwanza ambaye atafufuka kutoka ardhini. Yeye ndiye wa kwanza atayeombea na ndiye wa kwanza ambaye itaitikiwa du´aa yake. Yeye ndiye wa kwanza ambaye atabisha hodi kwenye mlango wa Peponi. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi ndiye wa kwanza nitayeitikiwa juu ya Pepo na ndiye Mtume wa kwanza aliye na wafuasi wengi.”

Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu wa Peponi ni safu 120 ambapo 80 katika hizo ni Ummah wangu na 40 zilizobaki ni nyumati zingine.”

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“70.000 katika Ummah wangu wataingia Peponi bila ya hesabu. Kila mmoja katika hawa 70.000 watakuja 70.000.”

Ameipokea Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 117-118
  • Imechapishwa: 23/10/2016