Paji la uso kugusa katika ardhi kwa mwenye kilemba


Swali: Inajuzu kusujudia kwenye kilemba ikiwa nimevaa kilemba au ni lazima paji la uso liguse kwenye ardhi moja kwa moja?

Jibu: Ikiwa kilemba kinakutia uzito kukivua, hakuna neno ukasujudia juu yake. Ama ikiwa hakikutii uzito kukivua, bila ya shaka kusujudia kwenye paji la uso ni jambo bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montqa--1431-03-06.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020