Mtume Muhammad ndio kiumbe cha kwanza kuumbwa?

Swali: Je, bwana wetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kiumbe cha kwanza cha Allaah au ni bwana wetu Aadam?

Jibu: Kiumbe cha kwanza katika watu ni Aadam (´alayhis-Swalaatu wa sallam) kwa maafikiano ya waislamu na udhahiri wa Qur-aan. Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwanaadamu kutokana na asli ya Aadam.

Kuhusiana na msemo wa baadhi ya wajinga ya kwamba Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kiumbe cha kwanza, ameumbwa kutoka kwenye nuru ya Allaah au kutoka kwenye nuru ya ´Arshi, maneno yake ni batili kabisa yasiyokuwa na msingi wowote wa usahihi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/307)
  • Imechapishwa: 24/08/2020