Swali: Je, inajuzu kuswali na hirizi au hapana?

Jibu: Wanachuoni wameafikiana juu ya uharamu wa kuvaa hirizi ikiwa sio ya Qur-aan na wakatofautiana ikiwa ni ya Qur-aan; kuna waliojuzisha kuivaa na wengine wakakataza kuivaa. Kauli inayosema kuwa haifai ina nguvu zaidi kutokana na ujumla wa Hadiyth na kuziba njia. Kujengea juu ya hilo ni jambo linalokuja nafasi ya mbele kabisa kutojuzu kuivaa wakati wa swalah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/212)
  • Imechapishwa: 24/08/2020