Swali: Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu: Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha. Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio lawajibu. Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
- Imechapishwa: 23/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja
Swali: Umetaja masharti na sunnah za kuchinja na hukutaja kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja. Ni ipi hukumu? Jibu: Kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja sio wajibu[1]. Mtu anaweza kuchinja kichinjwa chake ijapokuwa hakuelekea Qiblah. Lakini wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa bora zaidi ni mtu aelekee Qiblah. Kwa sababu ni ´ibaadah. Lakini…
In "Dhabh - Uchinjaji"
Kuacha Basmalah kabla ya kutawadha kwa kusahau
Swali: Nilitawadha na sikumbuki kuwa nilisema “Bismillaah” isipokuwa baada ya kumaliza kuosha mikono miwili. Nilipokumbuka nikarudi kutawadha upya. Ni ipi hukumu ya hilo? Jibu: Jopo la wanazuoni walio wengi wameonelea kuwa wudhuu´ unasihi pasi na kusema “Bismillaah”. Wanazuoni wengine wakaonelea kuwa ni lazima kusema “Bismillaah” ikiwa mtu anajua na amekumbuka…
In "Wudhuu´"
Amesahau Tasmiyah wakati wa kuchinja
Swali: Maneno ya Ibn ´Abbaas mwanzoni mwa mlango kuhusu mwenye kuacha kusema ”Bismillaah” kwa kusahau... Jibu: Ndio, hivo ndivo wanavoona kikosi cha wanazuoni kama vile maafikiano... Ibn Jariyr amesimulia maafikiano ya wanazuoni: رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا “Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1] Ni kama alivosema…
In "Dhabh - Uchinjaji"