Amesahau Tasmiyah wakati wa kuchinja

Swali: Maneno ya Ibn ´Abbaas mwanzoni mwa mlango kuhusu mwenye kuacha kusema ”Bismillaah” kwa kusahau…

Jibu: Ndio, hivo ndivo wanavoona kikosi cha wanazuoni kama vile maafikiano… Ibn Jariyr amesimulia maafikiano ya wanazuoni:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Ni kama alivosema al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) kwamba mwenye kuacha Tasmiyah sio fasiki. Maoni yanayosema kuwa mnyama anakuwa haramu ni dhaifu.

Swali: Vipi ikiwa mnyama hatikisiki isipokuwa jicho tu?

Jibu: Muhimu ni kwamba ni lazima kuhakikishwe kuwa mnyama yuko hai.

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24011/ما-حكم-ذبيحة-من-ترك-التسمية-ناسيا
  • Imechapishwa: 17/08/2024