Kumchinja mnyama punde kidogo tu kabla ya kufa

Swali: Vipi nikimchinja mnyama punde tu pale anapokaribia kukata roho?

Jibu: Kama alivosema (Ta´ala):

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ

“Mmeharamishiwa nyamafu [mzoga], na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah. Na [mnyama aliyeuawa] kwa kunyongwa, na [aliyekufa kwa] kupigwa, na kwa kuporomoka, na kwa kupigwa pembe [na mnyama mwengine], na aliyeliwa na mnyama mwitu [akafa] – isipokuwa mliyewahi kumchinja – na [pia mmeharamishiwa] waliochinjwa kwa ajili ya mizimu.” (05:03)

Muhimu utaje jina la Allaah ilihali bado yuko hai.

Swali: Hata kama ni muda mfupi tu kabla ya kufa?

Jibu: Ndio, haijalishi kitu. Muda wa kuwa yuko hai kwa namna ya kwamba mguu, kichwa au jicho likatikisika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24012/حكم-الذبيحة-التي-تذكى-وهي-قريبة-من-الموت
  • Imechapishwa: 17/08/2024