Swali: Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu: Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha. Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio lawajibu. Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
- Imechapishwa: 23/03/2018
Swali: Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu: Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha. Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio lawajibu. Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
Imechapishwa: 23/03/2018
https://firqatunnajia.com/kutoelekea-qiblah-wakati-wa-kuchinja-na-kusema-bismillaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)