Kuswali baada ya kunywa kinywaji cha kuleta uchangamfu (energy drink)


Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na kufanya ´ibaadah nyenginezo baada ya kutumia baadhi ya vitu vyenye kuleta uchangamfu na kuondosha uchovu na uvivu?

Ibn ´Uthaymiyn: Je, tembe hizi zinaondosha akili?

Muulizaji: Hapana. Zinamfanya mtu kuwa na uchangamfu tu.

Ibn ´Uthaymiyn: Kizuizi kiko wapi? Haina neno na wala haina tatizo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1760
  • Imechapishwa: 11/09/2020