Miji iliyozoea kuapa kwa jina la Mtume

Swali: Baadhi ya miji ndimi zao zimezowea kuapa kwa jina la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, wakemewe kwa kuendelea na jambo hilo?

Jibu: Ndio. Wabainishieni kuwa kitendo hicho hakifai. Haifai kuapa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuapwi isipokuwa kwa jina la Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kutaka kuapa basi aape kwa Allaah au anyamaze.”

“Msiape kwa baba zenu.”

Check Also

Ambaye alikuwa na zaidi ya wake wanne akifa anaswaliwa?

Swali: Mwenye kufa na yuko na wake watano au zaidi ni muislmu ambaye tuna haki …