Kufupisha katika safari ya pikniki

Swali: Tulitoka kwa ajili ya pikniki tukiwa na baadhi ya ndugu takriban masafa ya 120 km ilihali ni wenye kufupisha. Mmoja katika ndugu akasema kuwa hahisi utulivu wa nafsi kama hiyo ni safari na akaona kuwa bado ni mkazi. Matokeo yake akaswali kwa kukamilisha.

Jibu: Hapana. Sunnah ni yeye kuswali kwa kufupisha hata kama ni safari ya pikniki. Haya ndio maoni sahihi.

Swali: Lakini vipi ikiwa yeye anaona kuwa ni mkazi?

Jibu: Jambo ni jepesi. Akiswali kwa kukamilisha jambo ni jepesi. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akiswali kwa kukamilisha na kuna jopo la wengine walifanya hivo akiwemo ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alikamilisha. Kwa hivyo jambo ni jepesi. Hakika si venginevyo kufupisha ni bora peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21651/هل-تقصر-الصلاة-في-سفر-النزهة
  • Imechapishwa: 04/09/2022