Swali: Ni ipi hukumu ya kupandikiza mimba kwa njia ya kwamba yanachukuliwa manii ya mwanamme na kuwekwa kwenye kifuko cha uzazi cha mwanamke kupitia njia ya daktari?

Jibu: Jambo hili ni khatari sana. Ni nani ambaye anaweza kutoa dhamana kuwa daktari ataweka manii sahihi ndani ya kifuko cha uzazi wa mke wa mtu fulani? Kwa ajili hiyo naona kufunga kabisa mlango huo. Sitoi fatwa yoyote muda wa kuwa simjui mume, mke na daktari. Vinginevyo ni jambo linaweza kuwa na matokeo mabaya. Hili si suala jepesi. Kwa sababu ikiwa tutatokea udanganyifu hiyo ina maana ya kutokea mchanganyiko na vurugu katika nasaba za watu. Ni jambo limeharamishwa kwa mujibu wa Shari´ah kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke mjamzito asiingiliwe mpaka ajifungue kwanza.”[1]

Kwa hiyo mimi sitoi fatwa yoyote juu ya hilo. Labda kama ni qadhiya maalum ambapo nikamjua mume, mke na daktari.

[1] Abu Daawuud (2157) na at-Tirmidhiy (1564).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/25-26)
  • Imechapishwa: 04/09/2022