Swali: Kuna wanaosema kuwa pindi ninapomwita walii na kusema:

“Ee fulani! Niponye!”

Nasema hivo kwa mafumbo. Ninachokusudia ni:

“Ee fulani! Niombee kwa Allaah aniponye!”

Jibu: Kwa nini basi useme: “Niponye!”. Badala yake sema: “Nitibu!” iwapo ni tabibu. Kwa nini useme: “Niponye!”. Tabibu anatibu na wala haponyi. Anachofanya yeye ni kutoa dawa tu na wala haponyi. Kuponya kunatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Dawa ni sababu tu miongoni mwa sababu zingine. Usisemi tamko: “Niponye!” kumwambia kiumbe.

Swali: Tamko “Ee fulani! Niponye!” linazingatiwa kuwa ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu?

Jibu: Kwa hali yoyote ni kosa. Lakini ikiwa ana imani kuwa anaponya ndio inakuwa ni kumshirikisha Allaah. Ikiwa hana imani inahesabika ni kosa ambalo mtu anatakiwa kujiepusha nalo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (14) http://alfawzan.af.org.sa/node/2057
  • Imechapishwa: 23/04/2017