Msomaji akaanza kusoma kalima ya al-Albaaniy ambayo ilikuwa jawabu ya swali. Imerekodiwa na kuchapishwa katika gazeti[1]. Ninacholenga ni kwamba nimesikia taaliki ya Shaykh Ibn ´Uthaymiyn[2], na sisemi kuwa ni yenye faida peke yake, bali ambayo pia ni yenye umakini. Ni kitu ambacho wanazuoni wachache mno wanazinduka nacho. Kwa mfano mimi nawakosoa wanafunzi wengi, pengine wakawa ni miongoni mwa wale waliozama katika elimu, kwa sababu ya kuanza Khutbah na kalima zao kwa Khutbah ya Haajah kwa kuongeza juu ya yale yaliyopokelewa katika Sunnah Swahiyh, nayo ni:

“Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumtaka msaada na msamaha… “

Wanaongeza kwa kusema:

“Himdi zote njema anastahiki Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumtaka msaada na msamaha na uongofu… “

Nyongeza hii haikupokelewa katika matamshi ya Hadiyth. Hata hivyo wahubiri wa leo, akiwemo Khatwiyb wetu hii leo, ameongeza nyongeza hii. Mimi sina mazowea ya kuitaja, lakini msomaji huyu ameisoma kichwani mwake. Katika kanda ameongeza ziada hii. Hivyo Ibn ´Uthaymiyn akamsimamisha. Ni kitu ambacho kimenifurahisha. Amemrekebisha kwa sauti ya chini ambapo amekaribia kutosikiwa. Ni katika urafiki na adabu nzuri kwa mwanafunzi wake. Amemrekebisha. Msomaji akarudia na kusoma sentesi pasi na ziada “na uongofu”. Allaah amjaza kheri. Amemsahihisha na kumwelekeza.

Vivyo hivyo amemrekebisha makosa yake ya kisarufi aliokuwa akitumbukia mara nyingi alipokuwa anasoma.

Mfano mwingine ni ile Aayah iliyodaiwa, na sio ile Aayah iliyosomwa, ambapo nilisema kwamba ipo hekima nyuma ya maneno Yake Allaah:

وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ

“… na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini… ”[3]

Vinginevyo maana ingelikuwa imefahamika waziwazi, endapo Aayah ingelisomwa namna hii:

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu, basi Tutamgeuza alikogeukia… “

pasi na nyongeza hii:

وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ

“… na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini… ”

Inaonekana kwamba wale waliochapisha makala walidhani kuwa nilisahau kipande hicho, hivyo wakaitaja Aayah kama ilivyo ndani ya Qur-aan. Ilihali ambacho mimi nilikuwa nazungumzia ni kwamba kulikuwa kuna uwezekano Aayah ikaja pasi na nyongeza:

وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ

“… na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini… ”

Msomaji akaisoma Aayah kama ilivyokuja ndani ya Qur-aan. Shaykh akamzindua kwa mara nyingine. Allaah amjaze kheri. Hili pia ni katika umakini wake na umakini pia wa kuyaona makosa.

Mimi sijasoma makala hiyo katika kitabu. Umesoma kitabu?

Msikilizaji: Nimesoma kitabu.

al-Albaaniy: Je, nyongeza hii ipo?

Msikilizaji: Ndio.

al-Albaaniy: Hili ndio tatizo. Wamefanya makala maalum kutoka ndani ya kitabu na wakachapisha kitabu na bado kosa lipo. Lakini Shaykh – Allaah amjaze kheri – amelizindua hilo.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/al-albaaniy-kuhusu-mtawala-anayeweka-hukumu-zilizotungwa-na-watu-badala-ya-shariah/

[2] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-kwa-nini-khawaarij-hawayakubali-maneno-ya-ibn-abbaas/

[3] 04:115

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (940)
  • Imechapishwa: 19/10/2021