29. Matajiri kuchangia gharama za walima


27- Matajiri kuchangia gharama za walima

Imependekezwa kwa wale waliofunguliwa kuchangia katika maandalizi kutokana na na Hadiyth ya Anas juu ya kisa cha yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuoa Swafiyyah ambap alisema:

“Mpaka tulipokuwa njiani akamwandaa, yaani Umm Sulaym, kwa ajili yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamletea naye usiku. Kwa hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamka asubuhi akiwa na bibi harusi mpya na akasema: “Yule ambaye ana kitu basi akilete.” Katika upokezi mwingine: “Yule ambaye ana kitu cha ziada basi akilete.” Anas anaendelea kusimulia: “Kwa hivyo matandiko yakatandikwa na ikawa mtu mmoja analeta maziwa makavu, mwingine analeta tende, mwingine analeta samli safi; wakafanya al-Hays (mchanganyiko wa vitu hivyo vitatu). Wakaanza kula katika al-Hays hiyo na wanakunywa kwenye vidinbwi vya maji ya mvua. Hiyo ndio ilikuwa karamu ya ndoa ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim, Ahmad (03/102) na (195) na upokezi mwingine ni wake, Ibn Sa´d (08/122/123), al-Bayhaqiy (07/259), siyaaq ni yake na nyongeza ni ya Muslim (04/148).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 152
  • Imechapishwa: 21/03/2018