Mwanadamu akipewa na Allaah subira ni zawadi bora kabisa awezayo kupewa na ni zawadi ilio kunjufu zaidi. Ndio maana utamuona mtu mwenye subira pale atapoudhiwa na maneno ya kipuuzi ya watu, lau atasikia yenye kumchukiza na kumshambulia, utaona yuko namna hii. Hakasiriki na wala haghadhibiki kwa kuwa ni mwenye subira juu ya yale ambayo Allaah amempa mtihani kwayo. Ndio maana utaona moyo wake maishani ni wenye utulivu na starehe. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Hakuna yeyote aliyepewa zawadi bora na kunjufu zaidi kuliko subira.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/197)
  • Imechapishwa: 19/02/2023