Swali: Nina pesa ndani ya akaunti yangu ya akiba ninazotumia kukimu matumizi ya familia yangu? Je, ni lazima kuzitolea zakaah?
Jibu: Ndio, ni wajibu kuzitolea zakaah zikikamilisha mwaka. Kile ambacho zakaah inawajibika chenyewe kama chenyewe hakushurutishwi kwa mtu kuweka nia ya biashara. Kwa ajili hiyo ndio maana ni wajibu mavuno na nafaka yake kuvitolea zakaah hata kama mtu hakuyaandaa kwa ajili ya biashara. Kwa mfano mtu nyumbani kwake yuko na mitende inayofikia kile kiwango ambacho ni wajibu kutoa zakaah basi analazimika kuzitolea zakaah tende za mitende hii hata kama anapata ruzuku yake kupitia mitende hiyo. Hivyo hivyo ndio yanayosemwa juu vile vyengine vyote ambavyo ni wajibu kuvitolea zakaah ingawa mtu hakuviandaa kwa ajili ya biashara. Vilevile pesa ambazo ni wajibu kuzitolea zakaah ingawa mtu hakuziandaa kwa ajili ya biashara. Kwa hivyo mtu analazimika kuutolea zakaah mshahara wake ambao ameundaa kwa ajili ya matumizi yake muda wa kuwa umepitiwa na mwaka na pia umefikia kile kiwango cha wajibu kutoa zakaah.
Lakini hapa kuna suala ambalo linawatatiza watu wengi; mapato yanayopelekea kupanda na kushuka ndani ya muda wa mwezi, jambo ambalo linafanya inakuwa hajui ni wakati gani inawajibika kuyatolea zakaah. Ikiwa pesa hiyo inakuwa juu ya kile kiwango ambacho kinawajibisha kutoa zakaah kwa muda wa mwaka mzima, basi bora ni mtu azingatie kuanzia ile tarehe ya kwanza ambayo imefikia kile kiwango cha wajibu baada ya kuzihifadhi. Kisha atazitolea zakaah pesa hizo baada ya kukamilisha mwaka mmoja. Hiyo ina maana kwamba ile mali ambayo imezungukiwa na mwaka ameitoa zakaah ndani ya mwaka huo na mali nyingine yote iliyoongezeka ameitolea zakaah kwa kabla ya wakati wake, jambo ambalo halina ubaya. Mbinu hii ni nyepesi kwake kuliko kila mwezi kuutolea zakaah yake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/177-178)
- Imechapishwa: 18/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/177-178)
Imechapishwa: 18/06/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-ya-pesa-ya-akiba/