Swali: Ni ipi hukumu ya kuwa na hisa na makampuni? Ni ipi hukumu ya kukopa pesa kwa ajili ya kununua hisa? Je, hisa zinatolewa zakaah?

Jibu: kuweka hisa kwenye makampuni ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Kwa sababu baadhi namna wanavyoweka pesa katika kwenye benki za kigeni, au zinazofanana na kigeni, na wanazichukulia ribaa. Ikiwa ni sahihi basi ni haramu na ni dhambi kubwa kuweka hisa humo. Kwa sababu ribaa ni dhambi kubwa. Lakini ikiwa kampuni haiko namna hiyo na hakuna madhambi mengine katika sura hiyo, basi inafaa kuweka hisa ndani yake.

Ama mtu kuchukua mikopo ya ununuzi wa hisa ni upumbavu tu, ni mamoja amechukua mkopo kwa njia inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah au kwa njia ya ribaa. Kwa sababu mkopeshani hajui kama ataweza kulipa deni hilo katika siku zijazo au hatoweza. Ni vipi basi atajishughulisha dhimma yake na deni hili? Allaah (Ta´ala):

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ

“Wajizuie na machafu wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah awatajirishe katika fadhilah Zake.”[1]

Hakuwaamrisha watu hawa kuchukua deni, licha ya kwamba haja ya kuoa ni kubwa zaidi kuliko haja ya kuwa na pesa nyingi. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwataka mabarobaro wasioweza kuoa kuchukua mkopo, wala yule bwana ambaye hakupata angalau pete ya chuma kama mahari. Kwa msemo mwingine dini haipendezi kuchukua mkopo. Kwa ajili hiyo yule mtu ambaye anaijali dini na tetesi yake ajihadhari kuingia madeni.

Kuhusiana na namna ya kulipa zakaah ya hisa, dhimma ya mweka hisa inatakasika ikiwa serikali inachukua zakaah moja kwa moja kutoka kwenye hisa yake. Vinginevyo yeye mwenyewe anatakiwa kila mwaka kukadiria thamani yake na kutoa 2.5% juu yake. Hapo ni pale ambapo atakuwa amekusudia kwa hisa hiyo biashara. Lakini ikiwa kwa hisa hiyo amekusudia kuwekeza, basi haitolewi zakaah isipokuwa ikiwa faida hiyo ni kwa njia ya pesa na ikafikia kile kiwango ambacho inawajibikia kukitolea zakaah baada ya kukamilisha mwaka.

[1] 24:33

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/195-197)
  • Imechapishwa: 18/06/2026