70 – Khaythamah bin Sulaymaan ametukhabarisha: Ahmad bin Muhammad bin al-Hanaajir ametuhadithia: al-Haytham bin Humayd ametuhadithia … (ح) al-Hasan bin an-Nadhwr ametukhabarisha: Ishaaq bin Ibraahiym al-Baghdaadiy ametuhadithia: ´Umar bin Muusa ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (´Azza wa Jall):

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

“Basi Mola wako alipojidhihirisha katika jabali, akalifanya livurugike kuwa vumbi.”[1]

”Alionyesha (´Azza wa Jall) namna hii.”

Akaweka kidole gumba juu ya kidole kidogo.”[2]

al-Haytham ameongeza:

”Humayd alisema kumwambia Thaabit: ”Usitusimulie Hadiyth hii.” Thaabit akampiga kifuani na akamwambia maneno makali. Thaabit akasema: ”Anas ananisimulia nayo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha unanambia eti nisikusimulie nayo?”

[1] 7:143

[2] al-Haakim (2/320-321), ambaye ameisahihisha Hadiyth kwa mujibu wa masharti ya Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 88
  • Imechapishwa: 18/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy