31. Nyoyo zetu ziko baina ya vidole viwili vya Mola

68 – al-Hasan bin Muhammad bin an-Nadhwr ametukhabarisha: Ismaa´iyl in Yaziyd ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir ametuhadithia: Buswr bin ´Abdillaah ametuhadithia: Abu Idriys al-Khawlaaniy ametuhadithia: an-Nawwaas bin Sam´aan ametuhadithia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Hakuna moyo wowote isipokuwa uko baina ya vidole viwili vya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall). Akitaka kuunyoosha anaunyoosha, na akitaka kuupotosha, anaunyoosha.”

Akasema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثبت قلبي على دينكك

”Ee Mwenye kuipindua mioyo! Uthibitishe moyo wangu juu ya dini Yako.”

Akasema:

”Mizani iko kwenye mkononi mwa Mwingi wa rehama. Anainyanyua na kuishusha.”[1]

69 – al-Hasan bin Muhammad bin an-Nadhwr ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Yaziyd ametuhadithia: Khallaad bin Yaziyd ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Sinaan, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema:

يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثبت قلبي على دينكك

”Ee Mwenye kuipindua mioyo! Uthibitishe moyo wangu juu ya dini Yako.”

Kukasemwa: ”Ee Mtume wa Allaah! Utunakhofia juu yetu ilihali tumekuamini na kwa yale uliyokuja nayo?” Akasema: ”Hakika nyoyo ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa rehema. Anazipindua vile Anavyotaka.”[2]

Sufyaan ath-Thawriy akatikisa kidole cha kuashiria na kidole cha katikati.

Hadiyth hii imethibiti kwa maafikiano. Vivyo hivyo Hadiyth ya an-Nawwaas bin Sam´aan na imepokelewa na maimamu wanaotambulika na maimamu ambao haiwezekani kumtukana yeyote katika wao.

[1] Ahmad (4/282), Ibn Maajah (199) na ad-Daaraqutwniy katika “Kitaab-us-Swifaat” (45). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah (166).

[2] at-Tirmidhiy (2140), aliyesema Hadiyth ni nzuri. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2140).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 18/06/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy