62 – Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametukhabarisha huko Makkah: al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesimulia:
“Mwanachuoni wa kiyahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Ee Abul-Qaasim! Hakika Allaah atawaweka viumbe juu ya kidole, mbingu kwenye kidole, ardhi juu ya kidole, bahari juu ya kidole na udongo juu ya kidole.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana.” Ndipo Allaah (Jalla wa ´Azz) akashusha:
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ
”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itawekwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[1]
63 – Haajib bin Abiy Bakr at-Twusiy ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Haatim at-Twusiy ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur na Sulaymaan, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Ubaydah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
“Myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Hakika Allaah atazizuia mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya kidole, milima kwenye kidole, milima juu ya kidole na viumbe juu ya kidole.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana. Halafu akasema:
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ
“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria!”
Yahyaa bin Sa´iyd amesema: al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw amenihadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Ubaydah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka hali ya kushangazwa na kusadikisha.”[2]
64 – Abu ´Amr, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab bin Abiy Tammaam al-´Asqalaaniy ametuhadithia: Aadam ametuhadithia: Shaybaan ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Ubaydah, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:
“Kuna mwanachuoni mmoja wa kiyahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamwambia: “Ee Muhammad! Sisi tunakuta ndani ya Tawraat kuwa Allaah ataziweka siku ya Qiyaamah mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya kidole, mlima juu ya kidole, miti juu ya kidole, udongo juu ya kidole na viumbe vyengine vilivyobaki juu ya kidole. Kisha atazitikisa na kusema: “Mimi ndiye Mfalme.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana kwa ajili ya kusadikisha maneno ya mwanachuoni huyu. Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Hadiyth hii imethibiti kwa maafikiano.
65 – ´Abdur-Rahmaan bin Yahyaa na ´Abdullaah bin Ibraahiym wametukhabarisha: Abu Mas´uud ametuhadithia: Muhammad bin as-Swalt ametuzindua: Abu Kudaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Muslim bin Swubayh, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye ameeleza:
”Bwana mmoja wa kiyahudi alipita karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akamwambia: ”Tueleze, ee myahudi.” Akasema: ”Nakufikishia, ee Abul-Qaasim, ya kwamba Allaah ataiweka mbingu juu ya hii na ardhi juu ya hii.” Ndipo Allaah (Jalla wa ´Azz) akateremsha:

”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itawekwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”
66 – Abu ´Amr, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-´Asqalaaniy ametuhadithia: Aadam ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Abus-Saa-ib, kutoka kwa Abudh-Dhwuhaa, kutoka kwa Masruuq, ambaye ameeleza:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia myahudi: ”Nieleze kitu katika utukufu wa Allaah (Jalla wa ´Azz).” Akasema: ”Mbingu juu ya hiki (yaani kidole kidogo), ardhi juu ya hiki (yaani kidole cha pete), mlima juu ya hiki (yaani kidole cha katikati), maji juu ya hiki (yaani kidole cha kuashiria) na viumbe vyengine vyote kwenye hiki (yaani kidole cha gumba).” Ndipo Allaah akateremsha:

”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itawekwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume.”[3]
67 – Abu ´Amr, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ametuhadithia: Aadam ametuhadithia: Hammaad ametuhadithia, kutoka kwa Abu Sufyaan, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, ambaye amesema:
“Viumbe na ardhi zote katika mshiko wa Allaah (Jall wa ‘Azz) si zaidi ya punje ya haradali kwenye kidole cha pete cha mmoja wenu.”
[1] 39:67
[2] al-Bukhaariy (7414).
[3] Masruq bin al-Ajda´ alikuwa madhubuti, lakini hakuwahi kukutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hadiyth zilizotangulia kabla ya hizi mbili za mwisho zimepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim, kwa ajili hiyo mambo kama haya hayahitajiki.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 83-86
- Imechapishwa: 18/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 83-86
Imechapishwa: 18/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/30-mwanachuoni-wa-kiyahudi-na-kidole-kidoko-cha-allaah/