Swali: Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa hafungui masiku meupe, si akiwa safarini wala akiwa nyumbani.”

Je, hili limethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah?

Jibu: Hatufahamu usahihi wa riwaya hiyo. Bali lililothibiti kutoka kwake ni kwamba alikuwa wakati mwingine anafuatisha swawm mpaka ikasemwa hafungui na wakati mwingine anafuatisha kufungua mpaka ikasemwa hafungi. Hili ndilo limethibiti katika Hadiyth za Ibn ´Abbaas, ´Aaishah na wengineo kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo basi alikuwa wakati mwingine anazifunga siku hizo na wakati mwingine hafungi. Hata hivyo kufunga siku hizo ni Sunnah, kufungwa kwake ni Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa wakati mwingine anazifunga na wakati mwingine hushughulishwa nazo na hivyo akaziacha. Vivyo hivyo alikuwa akifunga siku za jumatatu na alkhamisi, lakini wakati mwingine alikuwa hushughulishwa na hivyo hafungi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1606/ما-صحة-حديث-كان-رسول-الله-لا-يفطر-الايام-البيض
  • Imechapishwa: 28/06/2026