Swali: Bwana mmoja hana mali nyingine zaidi ya malori ambayo anayakodisha. Je, anapaswa kuyatolea zakaah?
Jibu: Halazimiki kuyatolea zakaah. Magari makubwa sio mali ambayo inalazimika kuitolea zakaah, si yenyewe kama yenyewe wala thamani yake. Kwa sababu magari hayo yameandaliwa kwa ajili ya utumiaji na sio kwa ajili ya biashara. Kwa ajili hiyo yanaingia ndani ya maneno yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
”Muislamu halazimiki kumtolea zakaah mtumwa wala farasi wake.”[1]
Hata hivyo analazimika kutoa zakaah juu ya ile kodi yake baada ya kupita mwaka kuanzia kuandikwa kwa mkataba. Hukumu ni hiyohiyo juu ya mali nyingine yote ambayo haiwajibiki zakaah yenyewe kama yenyewe; sio wajibu kuzitolea zakaah ikiwa yameandaliwa kwa ajili ya utumiaji. Bali zakaah inatolewa juu ya yale mapato yake baada ya kupita mwaka kuanzia kuandikwe mkataba. Mfano wa mali isiyohamishika na vifaa. Kwa ajili hiyo sio wajibu kutoa zakaah juu ya ardhi za kilimo, hata kama zitakuwa nyingi, kinachotolewa zakaah matunda na mavuno yanayotokana nayo. Zakaah hii inalingana na mapato kutoka kwa vitu ambavyo ni vya kukodisha.
[1] al-Bukhaariy (1464) na Muslim (982).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/241)
- Imechapishwa: 06/05/2026
Swali: Bwana mmoja hana mali nyingine zaidi ya malori ambayo anayakodisha. Je, anapaswa kuyatolea zakaah?
Jibu: Halazimiki kuyatolea zakaah. Magari makubwa sio mali ambayo inalazimika kuitolea zakaah, si yenyewe kama yenyewe wala thamani yake. Kwa sababu magari hayo yameandaliwa kwa ajili ya utumiaji na sio kwa ajili ya biashara. Kwa ajili hiyo yanaingia ndani ya maneno yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
”Muislamu halazimiki kumtolea zakaah mtumwa wala farasi wake.”[1]
Hata hivyo analazimika kutoa zakaah juu ya ile kodi yake baada ya kupita mwaka kuanzia kuandikwa kwa mkataba. Hukumu ni hiyohiyo juu ya mali nyingine yote ambayo haiwajibiki zakaah yenyewe kama yenyewe; sio wajibu kuzitolea zakaah ikiwa yameandaliwa kwa ajili ya utumiaji. Bali zakaah inatolewa juu ya yale mapato yake baada ya kupita mwaka kuanzia kuandikwe mkataba. Mfano wa mali isiyohamishika na vifaa. Kwa ajili hiyo sio wajibu kutoa zakaah juu ya ardhi za kilimo, hata kama zitakuwa nyingi, kinachotolewa zakaah matunda na mavuno yanayotokana nayo. Zakaah hii inalingana na mapato kutoka kwa vitu ambavyo ni vya kukodisha.
[1] al-Bukhaariy (1464) na Muslim (982).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/241)
Imechapishwa: 06/05/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-ya-malori/