Swali: Ni vipi hisa zinatolewa zakaah, kama vile hisa za ardhi na kampuni?

Jibu: Inasemekana kuwa serikali huchukua zakaah kutoka katika mashirika kutegemea na ile rasilimali. Ikiwa ni sahihi, basi kile kinachokuliwa na serikali kinatosha na kinatakasa dhimma ya wenye hisa. Vinginevyo ni wajibu kutoa zakaah ya faida ya hisia baada ya kukamilika mwaka.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/200)
  • Imechapishwa: 16/05/2026