Swali: Je, mifugo wanaolishwa nusu mwaka wanatolewa zakaah?
Jibu: Mifugo wanaolishwa nusu mwaka mzima hawatolewi zakaah. Ili mifugo watolewe zakaah ni lazima kuwalisha mwaka mzima na zaidi ya hapo. Wale mifugo wanaolishwa nusu mwaka au chini ya hapo, hawatolewi zakaah. Isipokuwa ikiwa kama mifugo hao wameandaliwa kwa ajili ya biashara, basi hao watatolewa zakaah ya bidhaa za biashara. Katika hali hiyo kila mwaka kutakisiwa kisha kutolewe 2.5% ya thamani yake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/49)
- Imechapishwa: 16/05/2026
Swali: Je, mifugo wanaolishwa nusu mwaka wanatolewa zakaah?
Jibu: Mifugo wanaolishwa nusu mwaka mzima hawatolewi zakaah. Ili mifugo watolewe zakaah ni lazima kuwalisha mwaka mzima na zaidi ya hapo. Wale mifugo wanaolishwa nusu mwaka au chini ya hapo, hawatolewi zakaah. Isipokuwa ikiwa kama mifugo hao wameandaliwa kwa ajili ya biashara, basi hao watatolewa zakaah ya bidhaa za biashara. Katika hali hiyo kila mwaka kutakisiwa kisha kutolewe 2.5% ya thamani yake.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/49)
Imechapishwa: 16/05/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-ya-mifugo-wanaolishwa-nyasi-nusu-mwaka/