Swali: Ni vipi atatoa zakaah ya mali yake ambaye anaishi nje ya nchi? Je, aitume nchini mwake au katika ile nchi anayoishi? Au ateue mmoja katika wanafamilia yake wamtolee kwa niaba yake?

Jibu: Aangalie ni kipi chenye manufaa zaidi kwa wale wanaopewa zakaah. Ni sawa zaidi aitume nchini mwake au aitume katika nchi nyingine ambayo kuna mafukara? Ikiwa yanalingana hayo mawili, basi aitoe katika ule mji ambao anaishi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/315)
  • Imechapishwa: 25/04/2026