Je, utoaji wa zakaah umekomeka kwa nchi maalum?

Swali: Je, utoaji wa zakaah umekomeka kwa nchi maalum?

Jibu: Hapana. Allaah (Ta´ala) amewafanyia kikono wale watu wenye kuistahiki lakini si mahali pao. Amesema (Ta´ala):

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa]. Ni faradhi itokayo kwa Allaah; na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.”[1]

Hata hivyo hapana shaka yoyote kwamba bora zaidi ni mtu kuitoa zakaah pale alipo. Lakini ikiwa katika nchi alipo hakuna yeyote anayestahiki kupewa zakaah, basi anayo ruhusa ya kuitoa nje ya nchi.

[1] 09:60

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/314)
  • Imechapishwa: 25/04/2026