Swali: Ni ipi hukumu ya kuwapa zakaah wakimbizi na wahamiaji wa Kashmiyr kutokana na ufukara na kuhitaji kwao kukubwa?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanaona kufaa kuituma zakaah kwa waislamu ikiwa wana hali mbaya zaidi kuliko ile nchi ambayo mtu anaishi ndani yake. Katika hali hiyo baadhi ya wanazuoni wanashurutisha kuwa mtu aanze na ule mji ambao uko karibu zaidi na mtu. Lakini kile kinachonidhihirikia ni kwamba ikiwa katika nchi yake hakuna wale wahitaji wa zakaah, basi mtu aitume katika nchi za nje ambazo ni wahitaji zaidi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/317-318)
  • Imechapishwa: 25/04/2026