Ni kwa nini mtu anaenda na njia moja na kurudi na njia nyingine wakati wa kwenda kuswali ´iyd?

Swali: Ni ipi hekima ya kwenda na njia moja na kurudi na njia nyingine wakati wa kwenda kuswali ´iyd?

Jibu: Hekima kwa upande wetu kwanza ni kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwani kitendo hicho ni katika Sunnah.

Pili ni kudhihirisha nembo ya swalah ya ´iyd katika nchi mzima.

Tatu ni kwamba mtu anapata kuwaona wahitaji wote katika jamii.

Nne ni kwamba njia zote mbili zitamtolea ushuhuda siku ya Qiyaamah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/237)
  • Imechapishwa: 25/04/2026