Swali: Je, noti za leo zinatolewa zakaah na zinakuwa na ribaa?
Jibu: Noti za sasa zinachukua nafasi ya dhahabu na fedha. Kwa hiyo ni wajibu kuzitolea noti zakaah, kwa sababu watu hivi sasa wamezifanya noti hizi ndio badala ya dhahabu na fedha.
Kuhusu ribaa noti hizi zinakuwa na ribaa inapokuja katika mfumo wa ribaa ya mkopo na kuchelewesha (ربا النسيئة) na sio katika mfumo wa ribaa ya kuongeza (ربا الفضل) pale ambapo noti zinatofautiana. Kwa mfano hapana vibya kubadilishana sarafu tisa kwa noti kumi kwa sharti wakabidhiane papohapo kabla ya kutengana. Vivyo hivyo hukumu ni hiyohiyo ikiwa mtu anataka kubadilisha dola moja kwa 4 SAR; hapana vibaya kwa sharti wakabidhiane katika kikao hichocho.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/173)
- Imechapishwa: 13/06/2026
Swali: Je, noti za leo zinatolewa zakaah na zinakuwa na ribaa?
Jibu: Noti za sasa zinachukua nafasi ya dhahabu na fedha. Kwa hiyo ni wajibu kuzitolea noti zakaah, kwa sababu watu hivi sasa wamezifanya noti hizi ndio badala ya dhahabu na fedha.
Kuhusu ribaa noti hizi zinakuwa na ribaa inapokuja katika mfumo wa ribaa ya mkopo na kuchelewesha (ربا النسيئة) na sio katika mfumo wa ribaa ya kuongeza (ربا الفضل) pale ambapo noti zinatofautiana. Kwa mfano hapana vibya kubadilishana sarafu tisa kwa noti kumi kwa sharti wakabidhiane papohapo kabla ya kutengana. Vivyo hivyo hukumu ni hiyohiyo ikiwa mtu anataka kubadilisha dola moja kwa 4 SAR; hapana vibaya kwa sharti wakabidhiane katika kikao hichocho.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/173)
Imechapishwa: 13/06/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-na-ribaa-kwenye-noti/