Swali: Je, pete ya ndoa ni Bid´ah na khaswa wakati wa kufunga ndoa?
Jibu: Vile ninavoona ni kwamba pete ya ndoa dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza kwa sababu ni jambo linatoka kwa wasiokuwa waislamu. Kwa hali yoyote muislamu anatakiwa kujitukuza na asiigilize mambo kama haya. Ikiwa pete hiyo ya ndoa itaambatana na imani fulani kama wanavyoamini baadhi ya watu kwamba inamfungamanisha mke na mume, basi hukumu yake inakuwa mbaya na khatari zaidi. Pete haina taathira yoyote kabisa kwenye mahusiano kati ya wanandoa. Tumewaona wanandoa wenye kuvaa pete za ndoa lakini wanaishi maisha ya tabu na magomvi, sambamba na hayo kuna wengine wengi wasiovaa pete ya ndoa na wanaishi maisha mazuri na wake zao.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/112)
- Imechapishwa: 13/06/2026
Swali: Je, pete ya ndoa ni Bid´ah na khaswa wakati wa kufunga ndoa?
Jibu: Vile ninavoona ni kwamba pete ya ndoa dogo liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza kwa sababu ni jambo linatoka kwa wasiokuwa waislamu. Kwa hali yoyote muislamu anatakiwa kujitukuza na asiigilize mambo kama haya. Ikiwa pete hiyo ya ndoa itaambatana na imani fulani kama wanavyoamini baadhi ya watu kwamba inamfungamanisha mke na mume, basi hukumu yake inakuwa mbaya na khatari zaidi. Pete haina taathira yoyote kabisa kwenye mahusiano kati ya wanandoa. Tumewaona wanandoa wenye kuvaa pete za ndoa lakini wanaishi maisha ya tabu na magomvi, sambamba na hayo kuna wengine wengi wasiovaa pete ya ndoa na wanaishi maisha mazuri na wake zao.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/112)
Imechapishwa: 13/06/2026
https://firqatunnajia.com/dogo-liwezalo-kusemwa-kuhusu-pete-ya-ndoa/