Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na viatu?

Jibu: Kuswali na viatu ni Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akiswali ndani ya makubadhi yake, kama ambavyo hayo yamethibiti katika Hadiyth Swahiyh kupitia kwa Anas bin Maalik  (Radhiya Allaahu ´anh), kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Isitoshe amewaamrisha watu waswali ndani ya viatu vyao. Hata hivyo mtu asiswali ndani yake isipokuwa baada ya kuhakikisha kuwa havina najisi. Ikiwa ataona kuwa vina uchafu, basi atavisugua kwenye udongo mpaka uondoke halafu ndio aswali navyo.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/386)
  • Imechapishwa: 13/06/2026