Ni ipi hukumu ya anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu?

Swali: Ni ipi hukumu ya anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu?

Jibu: Inapendeza kutoa adhaana na kukimu kwa anayeswali peke yake na sio wajibu. Kwa sababu hakuna ambaye anamwita katika adhaana hiyo. Lakini kutokana na kwamba adhaana ni utajo na kumtukuza Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba mtu anajilingania mwenyewe kuswali na mafanikio, basi kitendo hicho kinapendeza. Isitoshe ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mola Wako anashangazwa na mchungaji wa mbuzi ambaye yuko juu ya mwamba wa jibali ambaye anaadhini kwa ajili ya swalah na anaswali. Allaah (´Azza wa Jall) anasema: “Mtazame mja wangu!  Anaadhini, nakimu swalah na ananiogopa. Nimemsamehe mja wangu na nimemwingiza Peponi.”[1]

[1] Abu Daawuud (1203), an-Nasaa’iy (1/108) na Ibn Hibbaan (260). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (1/1/102).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/161)
  • Imechapishwa: 13/06/2026