Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali swalah ya mamkizi ya msikiti wakati imamu anapoadhini? Zingatia pia kwamba hakuna muda wa kutosha wa kuswali Rak´ah hizo mbili baina ya adhanaa na Iqaamah?

Jibu: Bora ni kusubiri kuitikia kisha baada ya adhaana aseme:

اللَّهُمَّ ربَّ هَذه الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ والصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّداً الوسيلة والْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَاماً محموداً الذي وَعَدْتَهُ

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia na swalah iliosimama! Mpe Muhammad Njia (الوسيلة) na fadhilah, na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi.”[1]

Isipokuwa ikiwa ni katika swalah ya ijumaa; bora ni kuswali kwanza.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/193)
  • Imechapishwa: 13/06/2026