Swali: Ni kipi bora kwa mtu anapoingia msikitini na akamkuta imamu anaadhini?

Jibu: Bora ni yeye kumuitikia adhaana kisha baada ya hapo aombe kwa yaliyopokelewa. Baada ya hapo ndio aswali swalah ya mamkizi ya msikiti. Hata hivyo baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kwa ambaye ataingia msikitini na akamkuta imamu anaadhini adhaana ya ijumaa, basi atatakiwa aswali swalah ya mamkizi ya msikiti ili aweze kusikiliza Khutbah. Wamelitolea sababu jambo hilo kwamba kusikiliza Khutbah ni wajibu na kumuitikia kumuitikia muadhini sio wajibu – ni muhimu zaidi kuchunga jambo la wajibu kuliko kuchunga jambo linalopendeza.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/192-193)
  • Imechapishwa: 13/06/2026