Swali: Mtu kutoka katika masharifu analo deni. Je, inafaa kwake kuchukua swadaqah au zakaah?

Jibu: Anaweza kuchukua swadaqah lakini si zakaah. Anapewa kutoka katika swadaqah na si zakaah. Ikiwa ni kutoka ukoo wa wana wa Haashim, anapewa kutoka katika swadaqah na si zakaah.

Swali: Ikiwa kuna dharurah?

Jibu: Kama inafaa kwake kula nyamafu basi zakaah itakuwa ni halali kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24656/حكم-الزكاة-لرجل-من-الاشراف-عليه-دين
  • Imechapishwa: 22/11/2024