Swali: Mtu ambaye amechuua deni la ribaa kutoka katika benki kisha baadaye akafilisika na kushindwa kulipa. Je, apewe pesa ya zakaah?

Jibu: Ndio, apewe. Kwa sababu ni mwenye deni na anaingia ndani ya maneno ya Allaah (Ta´ala):

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

“Hakika si venginevyo zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao [kwa ajili ya Uislamu] na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri [aliyeharibikiwa]. Ni faradhi itokayo kwa Allaah; na Allaah ni Mjuzi, Mwenye hekima.”[1]

Kuhusu mtaji wa pesa yenyewe, ni jambo halina mashaka yoyote ndani yake. Ama kuhusu ile ribaa, kama tuko katika nchi ambayo tunaweza kufuta ribaa hii, basi hatutomsaidia, kwa sababu anaweza kujikwamua nayo. Na kama tuko katika nchi ambayo hatuwezi kufuta hiyo ribaa, basi ni lazima kwa huyo mdaiwa ailipe. Katika hali hiyo tutamsaidia. Haitakiwi kusema kwamba huku ni kusaidiana katika dhambi na uadui kwa sababu kimsingi ni kwamba dhambi zinamrejelea yule ambaye alichukua ribaa. Yule mwenye kuchukua ribaa amedhulumiwa na kwa ajili hiyo tunataka kumuokoa kutoka katika dhuluma hii. Maoni yangu juu ya maudhui haya ni kwamba ikiwa pande zote mbili watakubaliana juu ya mkopo wa ribaa kwa kuridhia kwao wote wawili, ni mamoja umepita kwa njia binafsi au ya benki, basi hatutompa ribaa yule mkopeshaji wala mkopeshwaji; ribaa hiyo tutaichukua na kuiweka katika wizara ya fedha, kwa sababu kila mmoja katika hawa wawili amemuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Haitakiwi kuwasaidia kumuasi.

[1] 09:60

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=ASO_iAxr1ww&list=UUPsMsuC6ZXFxOxYR0Qf_dhw
  • Imechapishwa: 07/12/2020